Tazama! Anakuja katika mawingu! Na kila jicho litamwona. Hata na wale waliomchoma mkuki na makabila yote ulimwenguni wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina. “Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “Aliyeko na aliyekuwako na ata kayekuja, Mwenyezi.”

Yohana Alivyopata Ufunuo

Mimi ni Yohana, ndugu yenu na mwenzenu katika mateso, na katika ufalme na subira kwa ajili ya Yesu Kristo. Niliwekwa katika kisiwa cha Patmo kwa ajili ya kutangaza neno la Mungu na kumshuhudia Yesu.

Read full chapter